Storm FM

Aliyemuua baba yake aachiwa huru Geita

24 September 2024, 4:54 pm

Muonekano wa Mahakama kuu ya Tanzania masjala ndogo ya Geita. Picha na Daniel Magwina

Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Geita imemuachia huru Mahele Petro (19), mkazi wa Nyamilembe wilayani Chato mkoani Geita baada ya kukiri kosa la kumuua baba yake kwa kumchoma mkuki shingoni bila kukusudia.

Na: Mwandishi wetu

Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 24, 2024 na Jaji Athuman Matuma, aliyesema Mahakama inamuachia huru mshtakiwa kwa sharti la kutotenda kosa la jinai kwa miezi 12.

Akisoma hukumu, Jaji amesema mshtakiwa alimuua baba yake mzazi, Petro Lyamba mkazi wa Kalebezo kwa kumpiga kwa mkuki shingoni kutokana na hasira zilizosababishwa na mgogoro wa kifamilia.

Amesema kutokana na hoja zilizojengwa na wakili wa mshtakiwa, Erick Lutehanga kama shufwaa kwa ajili ya nafuu ya adhabu imetiliwa maanani.