Mufti mkuu wa Tanzania autembelea mgodi wa GGML
18 September 2024, 1:32 am
Pichani ni mufti mkuu akiwa na viongozi wa dini mkoa na viongozi wa GGML .Picha na Adelina ukugani
Mufti na Sheikhe mkuu wa Tanzania amefanikiwa kutembelea mgodi wa GGML kwa mara ya kwanza uliopo mkoani Geita akiambatana na Viongozi mbalimbali wa Dini mkoani humo ili kujionea shughuli zinazofanywa na mgodi huo.
Na Adelina Ukugani.
Viongozi wa dini na waumini mkoani Geita wameshauriwa kutembelea sehemu mbalimbali ambazo ni muhimu katika uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla ili kujifunza zaidi fursa mbalimbali zitokanazo na maeneo hayo.
Hayo yamesemwa na mufti na sheikhe mkuu wa Tanzania Dkt Abubakari Zuberi Bin Ally Mbwana Jumanne Septemba 17, 2024, alipotembelea kampuni ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya Geita Gold Mining limited (GGML) pamoja na ujumbe alioambatana nao ili kujionea shughuli za mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na kampuni hiyo.
Ni sauti ya sheikhe mkuu wa Tanzania
Pichani ni mufti na viongozi wa Dini mkoa na kiongozi mmoja wa mgodi.Picha na Adelina ukugani.
Akizungumzia ushirikiano uliopo kati ya Mgodi wa GGML na ofisi ya BAKWATA mkoa wa Geita, Sheikh wa mkoa wa Geita Alhaji Yusuph Kabaju amesema Mgodi umekuwa mstari wa mbele katika kutoa ushirikiano na juhudi zinazofanywa na dini zote.
Ni sauti ya sheikhe wa mkoa wa Geita
Pichani ni Sheikhe wa mkoa wa Geita na Mufti mkuu.Picha na Adelina ukugani.
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa maendeleo wa Geita Gold Mining limited, Gilbert Moria ameshukuru kwa ziara hiyo na kueleza ushirikiano ulipo kwa taasisi na mgodi, huku Mariam Hammed Kasambo mwenyekiti wa Elimu habari na mawasiliano mkoani Geita (JUWAKITA) akitoa wito kwa wananchi na viongozi kutumia fursa zinazojitokeza.
Ni sauti ya Meneja mwandamizi wa maendeleo kampuni ya GGML
Pichani ni Meneja mwandamizi wa maendeleo katika mgodi huo.Picha na Adelina Ukugani.