Storm FM

BAKWATA yaibuka na matukio ya utekaji na mauaji nchini

16 September 2024, 6:12 pm

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akiwa katika baraza la maulid kitaifa mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na uwepo wa matukio ya watu kutekwa na wengine kuuawa makundi mbalimbali katika jamii yanalaani juu ya matukio hayo ikiwemo viongozi wa dini.

Na Mrisho Sadick:

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA limelaani vikali matukio ya utekaji na mauaji huku likiiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu wanaofanya vitendo hivyo nakuwachukulia hatua za kisheria.

Akitoa taarifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kwenye Baraza la Maulid Mkoani Geita lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Katibu Mkuu wa BAKWATA Al Haj Nuhu Mruma amesema kwa sasa vitendo viovu nchini vinaendelea kushamiri.

Sauti ya Katibu wa BAKWATA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wakazi wa Mkoa wa Geita kuwakemea baadhi ya watu wanaohatarisha amani ya nchi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mufti na shekhe mkuu wa Tanzania Dkt Abubakary Zubeir akiwa katika sherehe za maulid kitaifa mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakary Zubeir ameendelea kuwataka watanzania kudumisha amani nakulinda nchi.

Sauti ya Mufti wa Tanzania

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema serikali ipo macho Juu ya vitendo viovu huku akiwaomba Wananchi kushirikiana na serikali kukomesha vitendo hivyo.

Sauti ya Waziri Mkuu
Waumini wa dini ya kiislamu kutoka mikoa mbalimbali ya tanzania wakiwa katika maulid Mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kaulimbiu ya maadhimisho ya maulid mwaka huu ni “Maulid na aman zingatia maadili , uchumi , Shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa”