Storm FM

Mbuzi wa supu waibwa Geita

6 September 2024, 4:13 pm

Muonekano wa mfano wa zizi la mbuzi.

Watu wasiojulikana katika mtaa wa Mkoani mjini Geita wameiba mbuzi na kutokomea kusikojulikana jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za wananchi wafugaji.

Na: Kale Chongela – Geita

Wafugaji wa mbuzi waliopo katika mtaa wa mkoani kata ya kalangalala halmashauri ya mji wa Geita wamedai kulalamikia kuwepo kwa hali ya wimbi la wizi wa mbuzi katika mtaa huo.

Wakizungumza na Storm FM Septemba 04, 2024 baadhi ya wananchi pamoja na wafugaji katika mtaa huo wamesema kuwa changamoto hiyo imeibuka hivi karibu na kwamba suala hilo limeendelea kuwaathiri kiuchumi.

Sauti ya wananchi

Samson Joram ni mmoja ya wananchi walioibiwa mbuzi ambapo akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu ameeleza namna alivyopata taarifa ya kuibiwa mbuzi zake.

Sauti ya Samson Joram

Msimamizi wa polisi jamii katika mtaa huo Kasanga Gedion amekiri kupokea taarifa ya mbuzi kuibiwa na kwamba jitihada bado zinaendelea ili kubaini wanaojihusisha na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Sauti ya mkuu wa polisi jamii