Maulid kitaifa kufanyika mkoani Geita
6 September 2024, 7:53 am
Sherehe za Maulid ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume uhammad (SAW) ambayo huadhimishwa kila mwaka katika mwezi wa Rabiul Awwal kwenye kalenda ya kiislamu ambapo siku hii ilianza rasmi kusheherekewa katika karne ya 12.
Na: Kale Chongela – Geita
Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA mkoa wa Geita wanatarajia kufanya sherehe za Maulid kitaifa mkoani Geita katika viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari septemba 05, 2024 Sheikh wa mkoa wa Geita Alhaj Yusuph Kabaju amesema sherehe hizo zitafanyika Septemba 15-16, mwaka huu ambapo mkoa wa umepewa heshima kubwa ya kuandaa sherehe hiyo ambapo wageni mbalimbali watakuwepo akiwemo Sheikh mkuu wa Tanzania Muft Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana.
Katibu wa baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA mkoa wa Geita Abas Mtuguja amebainisha kuwa sherehe hiyo itaambatana na uwepo wa maonesho ya wajasiriamali katika uwanja wa CCM Kalangalala ambayo yataanza Septemba 07, 2024.