Storm FM

Mkoa wa Geita wavuka lengo zoezi la uandikishaji

21 August 2024, 4:24 pm

Afisa mwandikishaji akichukua taarifa kutoka kwa mwananchi katika zoezi la uandikishaji kwenye kituo cha shule ya sekondari Kalangalala.

Wananchi mkoani Geita wameitikia wito kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji a uboreshaji wa taarifa za mpiga kura mkoani Geita.

Na: Kale Chongela – Geita

Mkoa wa Geita umevuka lengo katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ambapo jumla ya wapiga kura wapya 368,100 wameandikishwa .

Akizungumza na Storm Fm Agosti 20, 2024 akiwa ofisini kwake mratibu wa zoezi la uandikishaji mkoa wa Geita Bw. Herman Matemu amesema mkoa wa Geita umefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika zoezi hilo kwani makadirio ya awali ilikuwa kuandikisha wananchi 229,672.

Sauti ya mratibu

Aidha ameongeza kwa kubainisha kuwa licha ya zoezi hilo kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, jumla ya wananchi 313 wamefutiwa taarifa zao kutoka na sababu mbalimbali.

Sauti ya mratibu

Baadhi ya wananchi halmashauri ya mji wa Geita kwa nyakati tofauti wamepongeza hatua hiyo na kueleza kuwa itawasaidia kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani 2025.

Sauti ya wananchi

Ikumbukwe kuwa mkoa wa Geita ulianza zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura Agosti 5 hadi 11 mwaka huu 2024.