Storm FM

Kijana apewa kichapo kwa tuhuma za kuiba Tsh. 70,000 Katoro

14 August 2024, 11:28 am

Shughuli mbalimbali zikiendelea katika soko la CCM lililopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro. Picha na Nicolaus Lyankando

Soko la CCM ni soko mama lililopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro ambalo limekuwa likitumiwa na watu kutoka katika vijiji vya Magenge, Nyamalulu, Kaseme, Kasesa, Mabamba nk

Na: Nicolaus Lyankando – Geita

Kijana mmoja ambaye hakufahamika jina lake wala makazi yake amenusurika kifo baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali akidaiwa kumuibia mteja wa sokoni hapo kiasi cha shilingi elfu sabini.

Tukio hilo limetokea Agosti 11, 2024 majira ya saa tano asubuhi ambapo baada ya kupigwa na wananchi hao alikimbilia katika kituo cha afya Katoro kwaajili ya kujinasua.

Sauti ya mashuhuda

Wakiongea na Storm Fm wafanya biashara wa soko hilo wamesema kijana huyo baada ya kugundulika kufanya hivyo walianza kumshushia kipigo huku wakielezea undani wa tukio hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya maadili katika soko la CCM amewataka wafanya biashara wa soko hilo kujilinda na mali zao wakati wa mchana kwani ulinzi uliopo sokoni hapo ni wa usiku tu.

Sauti ya mwenyekiti