Storm FM

TAKUKURU Geita kufanyia uchunguzi miradi yenye mapungufu

1 August 2024, 2:42 am

Naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Alex Mpemba akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Geita imeendelea kufanya uchunguzi wa miradi mbalimbali ili kubaini iwapo kuna ubadhirifu au ukamilifu wa miradi hiyo.

Na: Kale Chongela – Geita

Jumla ya kesi 19 za vitendo vya Rushwa zilizokuwa zikiendelea katika Mahakama mbalimbali Mkoa wa Geita kati ya hizo mbili zilitolewa maamuzi na Jamhuri ilishinda.

Kauli hiyo imetolewa na naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Alex Mpemba Julai 30 mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni, 2024.

Amesema katika kipindi cha April hadi Juni TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa miradi 25 ya maendeleo na kati ya hiyo miradi 5 imebainika kuwa na upungufu wa kukosa ubora.

Sauti ya naibu mkuu TAKUKURU Geita

Aidha amebainisha kuwa TAKUKURU imeanza kuchunguza upotevu wa baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa na kupokelewa katika hospitali ya Katoro ambapo vifaa hivyo vimeonekana kupokelewa lakini havionekani wala kutumika na pia kutoonekana katika stoo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoa wa Geita wakiendelea na mahojiano. Picha na Kale Chongela

Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nchini.

Sauti ya naibu mkuu TAKUKURU Geita