Storm FM

Mameneja TANESCO kanda ya ziwa wakutanishwa

27 July 2024, 12:13 pm

Mameneja TANESCO kanda ya ziwa wakiwa katika kikao kazi. Picha na Edga Rwenduru

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati nchini (EWURA)imewakutanisha mameneja wa TANESCO mikoa ya kanda ya ziwa kwaajili ya kujadili uboreshaji wa huduma.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba watumiaji wa nishati ya umeme ikiwemo kukatika mara kwa mara, mamlaka ya udhibiti wa huduma ya nishati na maji nchini EWURA kanda ya ziwa imefanya kikao kazi na wataalamu na mameneja wa TANESCO kutoka mikoa yote ya kanda ya ziwa ili kuboresha huduma kwa wateja.

Kikao hicho kimefanyika Julai 26, 2024 katika ukumbi wa The Giant Hotel ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Katoro ambapo pia wamejadili namna ya kutekeleza maagizo ya waziri wa nishati na Naibu waziri mkuu Dkt. Dotto Mashaka Biteko aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa taarifa za sekta ya nishati jijini Dodoma ambapo EWURA na TANESCO waliingia mkataba wa utendaji kazi.

Meneja wa EWURA kanda ya ziwa George Mathew akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Edga Rwenduru

George Mathew Mhina ni meneja wa EWURA kanda ya ziwa anaeleza juu ya kikao hicho.

Sauti ya meneja EWURA

Gibons Mwaipungu ni kaimu meneja TANESCO mkoa wa Kagera na Tarikisio Chafumbwe ni kaimu meneja mkoa wa Mara wanabainisha umuhimu wa kikao kazi hicho.

Sauti ya mameneja Kagera na Mara
Meneja wa TANESCO mkoa wa Geita Joachim Ruweta akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Edga Rwenduru

Meneja wa TANESCO mkoa wa Geita Joachim Ruweta amesema TANESCO mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Jeshi la polisi wameanza msako wa kuwabaini wanaoiba nyaya za Transfoma.

Sauti ya meneja TANESCO Geita