Storm FM

Wezi wabomoa tofali na kuiba, wajenga upya Geita

25 July 2024, 10:49 am

Mwonekano wa ndani eneo ambalo limebomolewa na wezi na kuiba. Picha na Amon Mwakalobo

Matukio ya baadhi ya watu kupora mali na kuiba yameendelea kuwa changamoto hususani kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiibiwa mali zao.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Watu wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa ni wezi wamebomoa kibanda cha biashara cha mkazi wa mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita na kuiba mali za zaidi ya shilingi laki sita.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Julai 24, 2024 ambapo mmiliki wa kibanda hicho anayejulikana kwa jina la Mama Chris ameeleza namna alivyokuta eneo lake la kazi limeibiwa

Sauti ya mmiliki wa kibanda
Mwonekano wa nje eneo ambalo wezi wamebomoa na kuiba. Picha na Amon Mwakalobo

Kwa upande wa majirani wa eneo hilo ambao pia ni wafanyabiashara wameelezea jinsi wanavyosumbuliwa na wezi kwenye biashara zao.

Sauti ya mashuhuda

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Enos Cherehani amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi suala zima la ulinzi na usalama mtaani hapo.

Sauti ya mwenyekiti