Storm FM

GEUWASA, RUWASA zapewa maelekezo juu ya miradi ya maji

23 July 2024, 7:33 am

Mkurugenzi wa GEUWASA Frank Changawa (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo wa naibu waziri wa maji Mathew Kundo. Picha na Kale Chongela

Wizara ya maji nchini imedhamiria kukamilisha miradi yote ya maji ambayo imeanzishwa ili wananchi wote wapate huduma ya maji safi na salama.

Na: Kale Chongela -Geita

Naibu waziri wa maji mhandisi Kundo Mathew ameutaka uongozi wa GEUWASA NA RUWASA kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara katika ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28  unaojengwa katika kijiji cha Senga kata ya Senga wilayani na Mkoani Geita.

Mradi wa maji wa miji 28 unaoendelea kujengwa katika kijiji cha Senga mkoani Geita. Picha na Kale Chongela

Mhandisi kundo amesema hayo Julai 20, 2024 akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita baada ya kutembelea mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya AFCONS kutoka nchini India ambapo amesema mradi huo umefikia asilimia 18% ya ujenzi wake wenye thamani ya Bilioni 124.

Sauti ya naibu waziri wa maji

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita (GEUWASA) Frank Changawa amesema mradi huo ukikamilika utahudumia vijiji 19 katika wilaya ya Geita pamoja na kata zote 13 za halmashauri ya Mji wa Geita.

Sauti ya mkurugenzi GEUWASA