Storm FM

Ashangaza majirani kwa kuhifadhi taka ndani Msalala Road

3 July 2024, 9:58 am

Elia Mayoyo ambaye amehifadhi uchafu katika chumba chake anacholala. Picha na Amon Mwakalobo

Suala la usafi wa mazingira ni jambo ambalo linahimizwa na viongozi kwa jamii kuzingatia ili kuweza kujiepusha na maradhi mbalimbali.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Mwanaume mmoja kwa jina Elia Mayoyo (51) mkazi wa mtaa wa Msalala Road halmashauri ya mji wa Geita amewashangaza majirani na wakazi wa mtaa huo kwa kukutwa na rundo la taka na uchafu ndani ya chumba chake cha kulala huku akikiri kutunza taka hizo ndani ya chumba chake.

Tukio hilo limetokea Julai mosi, mwaka huu na kwa mujibu wa majirani na wamiliki wa nyumba anayoishi mwanaume huyo, ni kwamba amekaa kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na alipotakiwa kuondoka aligoma hivyo kutolewa kwa amri ya mahakama na ndipo akakubali kuhama na kuanza kutoa mizigo yake nje zikiwemo taka na uchafu.

Sauti ya majirani

Kwa upande wake Elia amesema taka hizo pamoja na uchafu mbali mbali kikiwemo kinyesi cha popo amevikusanya kwa muda mrefu baadaye aje afanye biashara ya kuuza mbolea ya asili ya kinyesi cha popo na siso.

Sauti ya Elia Mayoyo
Taka ambazo zimehifadhiwa ndani na Elia Mayoyo. Picha na Amon Mwakalobo

Balozi wa eneo hilo Bi. Angelina Gervas amesema wao hawana cha kufanya kwani aliyekuwa anakusanya uchafu inawezekana ameona una manufaa kwake ndo maana ameamua kufanya hivyo.

Sauti ya balozi

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Sostenes Kalist ameshangazwa na tukio hilo na kuwaomba wanajamii kuzingatia usafi kwani kwa kile alichokifanya Elia kinahatarisha hata afya yake mwenyewe.

Sauti ya mwenyekiti