Storm FM

Mwenyekiti mtaa wa Mwatulole auwawa na watu wasiojulikana

24 June 2024, 4:33 pm

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Matukio ya ukatili ikiwemo vitendo vya mauaji bado ni changamoto kwa baadhi ya mkoani Geita hali inayozua hofu kwa wananchi.

Na: Kale Chongela – Geita

Mwenyekiti wa mtaa wa Mwatulole uliopo kata ya Buhalahala mjini Geita, Noel Ndasa ameuawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali mwilini na watu wasiojulikana.

Tukio hilo limetokea Juni 23, 2024 majira ya saa mbili usiku, baada ya wanaume wawili kufika nyumbani kwake, wakidai wanataka huduma ya kupewa kibali cha kusafirisha mifugo.

Akisimulia tukio hilo, mtoto wa marehemu ameeleza namna watu hao walivyofika nyumbani na kumuulizia baba yao hadi kutekeleza tukio hilo.

Sauti ya mtoto wa marehemu
Baadhi ya ndugu, marafiki na majirani waliojitokeza kwenye msiba nyumbani kwa marehemu. Picha na Kale Chongela

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea na mpaka sasa hakuna aliyekamatwa kuhusishwa na tukio hilo na kwamba baadaye taarifa rasmi itatolewa.

Sauti ya kamanda wa polisi