Storm FM

DC Geita akemea migogoro ya wakulima na wafugaji

22 June 2024, 3:33 pm

Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mpomvu. Picha na Kale Chongela

Migogoro ya wakulima na wafugaji hutajwa kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo katika jamii za wafugaji na wakulima, jambo ambalo viongozi hukemea vikali.

Na: Kale Chongela – Geita

Wakazi wa mtaa wa Mpomvu kata ya Mtakuja mjini Geita wameiomba serikali ya wilaya ya Geita kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji kufuatia kuwepo kwa hali ya baadhi ya wakulima kupigwa na wafugaji.

Wameeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Juni 21, 2024 mbele ya mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba ambapo baadhi ya wakulima wameeleza kuwa pamekuwepo na changamoto ya baadhi yao kupigwa na wafugaji hasa wanapo wabaini kuwa wamelisha mifugo kwenye mashamba yao.

Sauti ya wakulima
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita Yefred Myenzi akizungumza katika mkutano. Picha na Kale Chongela

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita Bw. Yefred Myenzi ametumia fursa hiyo kuwataka wafugaji kuzigatia kanuni bora za ufugaji ili kuondoa changamoto hizo.

Sauti ya mkurugenzi

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara. Picha na Kale Chongela

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba amemuugiza afisa mifugo kufika katika eneo hilo na kutatua mgogoro huo kabla haujaleta madhara makubwa kati ya wakulima na wafugaji.

Sauti ya mkuu wa wilaya