Transfoma yalipuka na kuzua taharuki Mbugani
21 June 2024, 10:29 am
Wananchi wa mtaa wa Mbugani mjini Geita wamekumbwa na taharuki baada ya transifoma iliyopo katika mtaa huo kupata hitilafu na kushika moto hali iliyopelekea kukatika kwa umeme katika eneo hilo.
Na: Evance Mlyakado – Geita
Tukio hilo limetokea usiku wa Juni 20, 2024 ambapo wananchi wameeleza kuwa sio tukio la kwanza kutokea katika mtaa huo katika transfoma hiyo hiyo kwani limekuwa lijijirudia na hivyo wameiomba serikali kupitia shirika la umeme Tanesco mkoa wa Geita kutatua changamoto hiyo
Mwenyekiti wa mtaa wa Mbugani John Joachim John amethibitisha kutokea kwa changamoto hiyo katika mtaa wake na kwamba imekuwa ikijirudia licha yakuwatafuta wahusika wa Tanesco kwani wamekuwa wakichelewa kufika kwa wakati
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita kupitia kwa Afisa habari wake Staff Sajenti Bahati Lugodisha limethibitisha kufika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto uliokuwa ukiwaka katika transfoma hiyo kwa ushirikiano na wataalamu kutoka Tanesco ambapo afisa uhusiano na huduma kwa wateja Lucas Swere amesema uchunguzi utafanyika ili chanzo kamili.