Storm FM

Anusurika kifo kwa kichapo baada ya kumtapeli wakala Chato

10 June 2024, 3:34 pm

Picha na mtandao (google)

Matukio ya utapeli wa fedha yanaendelea kushamiri kwa sura tofauti tofauti licha ya jitihada za serikali kuendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na matukio hayo.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Mwanaume mmoja ambaye hajafahamika jina wala sehemu alipokuwa akitokea amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali katika kitongoji cha Bukiriguru kijiji cha Nyabilezi kilichopo kata ya Bukome wilayani Chato mkoani Geita mara baada ya kutapeli kiasi cha shilingi laki sita mali ya Melina Bulenganija Kaniki mfanyabiashara ya uwakala wa kutoa na kuweka pesa katika mitandao ya simu. 

Tukio hilo limetokea Juni 06, 2024, akizungumza na Storm FM Bi. Melina ambaye anaishi na changamoto ya ulemavu wa miguu yote miwili amesema kuwa mwanaume huyo alikwenda kupata huduma kama mteja wa kawaida ambapo baadaye aliomba simu ya wakala huyo kutaka kujiridhisha kama kweli jina na kiwango kilichotumwa ni halisi na baada ya kushika simu ya wakala ndipo alipojihudumia kiasi cha shilingi laki sita.

Sauti ya wakala

Baadhi ya wananchi Deus William na Faida Juma miongoni mwa waliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wameeleza namna walivyofanikiwa kumkamata

Sauti ya wananchi

Mwenyekiti wa kitongoji cha Bukiriguru Juma Bunzali kutoka katika kijiji hicho cha Nyabilezi amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo na kuwaasa wananchi kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa za kwa uongozi juu ya matukio hayo

Sauti ya mwenyekiti

Jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio kisha kumchukua mtuhumiwa na kumpeleka kituo cha polisi Chato kwa utaratibu na hatua zaidi.