Wadaiwa sugu wa pango la ardhi kufikishwa mahakamani Geita
17 May 2024, 10:16 am
Serikali mkoani Geita imekusudia kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu walioshindwa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa hiari huku ikiwataka kulipa madeni yao ndani ya siku 30 ili kuepuka mkono wa sheria.
Kauli hiyo imetolewa na kamishna msaidizi wa ardhi mkoa wa Geita ambapo amesema watu wanaomiliki viwanja na mashamba yaliyopimwa ambao hawajalipa kodi ya ardhi wanatakiwa kufanya hivyo haraka kuepuka kuangukia kwenye mikono ya sheria.
Maafisa ardhi wateule kutoka halmashauri ya wilaya na mji wa Geita wameahidi kufanya kazi usiku na mchana kuwahudumia wananchi watakaofika katika ofisi hizo kulipa madeni yao.
Malengo ya makusanyo ya kodi ya ardhi kwa mkoa wa Geita mwaka huu wa fedha ni Bilioni 4.8 lakini mpaka sasa wamekusanya Bilioni 1.2 kikiwa ni kiasi kidogo ukilinganisha na muda uliyosalia.