Taka ni kikwazo kwa baadhi ya maeneo mjini Geita
1 May 2024, 3:43 pm
Licha ya jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na halmashauri ya mji wa Geita ili kukabiliana na uchafu wa mazingira, bado hali ni tete kwa baadhi ya maeneo.
Na: Kale Chongela – Geita
Baadhi ya wananchi kutoka mitaa ya Mpomvu, Mbabani, Nyantorotoro ubaoni, Kivukoni na soko la mbagala wameeleza uwepo wa changamoto ya taka kutoondolewa kwa wakati licha ya kujaa kwenye makazi yao na maeneo ya biashara hali ambayo inasababisha hofu juu ya magonjwa ya mlipuko
Balozi wa mtaa wa Kivukoni Bw. Elias Mfungo ameeleza hatua ambazo wanaendelea kuchukua ili kukabiliana na changamoto hiyo
Afisa mazingira kutoka halmashauri ya mji wa Geita Edward Mwita ameeleza namna wanavyofanya kazi na kuelezea changamoto ya magari kuchelewa kuondoa taka kwa wakati
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Halmashauri ya Mji wa Geita ina jumla ya wakazi 361,671 .