Umoja wa madereva bajaji mji wa Katoro wakutana
25 April 2024, 10:04 am
Usafiri wa pikipiki zenye magurudumu matatu maarufu bajaji nchini umekuwa ukitegemewa na wananchi kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya maeneo nchini huku baadhi ya vijana wakijiajiri na kuweza kuendesha maisha yao.
Na Evance Mlyakado – Geita
Umoja wa waendesha bajaji ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Katoro umeitisha mkutano wake na wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya usafirishaji lengo ikiwa ni kujadili mambo muhimu yanayoukabili umoja huo.
Katika mkutano huo changamoto mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo madereva bajaji kubeba abiria juu ya kiwango ambacho kinatakiwa pamoja na ukosefu wa leseni kwa madereva jambo ambali linachangia kuongeza ajali za barabarani.
Katika mkutano huo wadau mbalimbali wa usafirishaji wakiwemo mamlaka ya usafirishaji ardhini nchini LATRA, Jeshi la polisi na viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita walihudhuria na kutoa elimu kuhusu usafirishaji kama anavyoeleza afisa mfawidhi kutoka LATRA Bw. Rajab Suleiman
Kwa Upande wake mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashimu A. Komba amewaasa waendesha bajaji wote ambao hawajajiunga na umoja huo kujiunga huku akiwataka viongozi kuwasaidia vijana hao katika utatuzi wa changamoto zao.
Katika hatua nyingine DC Komba amewashauri kuzingatia suala la bima za Afya ili ziweze kuwasaidia pindi wanapopitia changamoto ikiwemo kupata ajali