Viongozi wa dini waonya serikali kulaumiwa kwa majanga ya asili
16 April 2024, 9:05 pm
Kuendelea kutokea kwa majanga ya asili hapa nchini baadhi ya wananchi wameanza kuinyoshea kidole serikali huku baadhi ya viongozi wa dini wakionya.
Na Nickolaus Lyankando – Geita
Watanzania wametakiwa kuacha tabia ya kuilaumu serikali kutokana na majanga ya asili ambayo yanatokea hususani mafuriko nabadala yake waungane kwa pamoja kuliombea taifa ili kuepuka majanga hayo.
Kauli hiyo imetolewa na Askof wa makanisa ya Presbterian,central mission of Africa PCMA nchini Tanzania Bishop Mondeha Kabeho katika kongamano la siku nne la kuliombea taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan lililofanyika katika Kanisa la Mlima wa Moto katoro Mkoani Geita.
Sauti ya Askofu Mondeha Kabeho
Kwa upande wake Nabii kiongozi wa kanisa la mlima wa moto katoro Meshack mpanduji amewaomba watanzania kuacha kubeza shughuli zinazofanywa na serikali nabadala yake waiunge mkono kwa kazi inayofanya.
Sauti ya Nabii Meshack Mpanduji
Nao baadhi ya manabii kutoka madhehebu Mbalimbali hapa nchini waliohudhuria katika kongamano hilo pamoja na waumini wameahidi kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita katika mapambano dhidi ya maadui wa taifa.
Sauti ya baadhi ya waumini na Manabii
Kongamano hilo la Maombi limewakuatanisha zaidi ya manabii 18 wa makanisa ya PCMA kutoka hapa nchini.