TEMESA kujiendesha kisasa kuondoa malalamiko
8 December 2023, 1:37 pm
TEMESA kujivua gamba ili kwendana na kasi ya teknolojia kwa kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa utendaji kazi ili kuondoa malalamiko kwa wadau wake.
Na Mrisho Sadick – Geita
Wakala wa ufundi na umeme Tanzania (TEMESA) umekusudia kujiendesha kisasa kwa kufanya mabadiliko kwenye mifumo na utendaji kazi hususani kwenye manunuzi ya vipuri na vilainishi.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala amebainisha hayo baada ya kupokea changamoto mbalimbali Juu ya utendaji kazi usiyoridhisha katika kikao cha wadau wa TEMESA cha kujadili changamoto zilizopo ili zipatiwe ufumbuzi kilichofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita.
Katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Herman Matemu amesema mabadiliko ambayo yamefanywa na TEMESA kwenye upande wa TEHAMA , Ufundi na Umeme itakuwa fursa kwao.
Baadhi ya wadau wa TEMESA akiwemo Mganga Mkuu wa wilaya ya Bukombe Dkta Deograsia Mkapa na Afisa usafirishaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Juma Jilala wamesema bado TEMESA inakabiliwa na changamoto nyingi nakwamba kupitia mabadiliko hayo huenda wakaongeza ufanisi katika utenda utendaji kazi wao.