Matokeo ya sensa ikawe chachu ya kuwaletea wananchi maendeleo
19 October 2023, 11:09 am
Kujulikana kwa idadi ya watu na makazi kupitia Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ikawe chachu ya viongozi wa serikali kupanga mikakati ya maendeleo kwa wananchi wake.
Na Mrisho Sadick:
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka viongozi na wataalamu Mkoani humo kutumia takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kubuni nakutekeleza mikakati itakayo saidia kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja.
Mhe Shigela ametoa kauli katika semina ya siku moja ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita huku Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu akisema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupanga mikakati ya maendeleo kwa wananchi.
Awali Akizungumza katika semina hiyo Meneja takwimu Kutoka Ofisi ya Taifa ya takwimu Mkoa wa Geita Khalid Msabaha amesema serikali imekamilisha Ripoti 11 za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Takwimu za sensa zinaonesha kuwa matumizi ya Kuni na mkaa kwa wakazi wa Mkoa wa Geita ni asilimia 54.3 nyuma ya Mkoa wa simiyu ambao unamatumizi kwa asilimia 77 huku wadau wa semina hiyo wakiiomba serikali kuchukua hatua za haraka.