Watu watatu wafariki kwa ajali Geita, wawili watumishi wa serikali
9 October 2023, 6:03 pm
Ajali za barabara zimeendelea kukatisha uhai wa watu wengi , jitihada za makusudi zinahitajika ikiwemo elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kupunguza matukio hayo hususani kwa waendesha pikipiki.
Na Mrisho Sadick – Geita
Watu watatu wakiwemo watumishi wawili wa serikali wamefariki Dunia baada ya kugongwa na Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T402 AUB katika Mtaa wa Magogo Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita.
Tukio hilo limetomea usiku wa kuamkia Oktoba 08,2023 wakati watu hao walipokuwa wamebebana kwenye usafiri wa Pikipiki yenye namba za usajili MC 576 BBK ndipo wakagongwa na Gari hilo walipokuwa wakijaribu kukata kona ya Kuelekea majumbani kwao nakufariki papo hapo.
Waliofariki katika ajali hiyo ni Upendo Danda Afisa serikali za mitaa mwandamizi Idara ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita , Emmanuel Mao Mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapo awali alikuwa Mtumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Yusuph Yohanes ndugu wa marehemu wa Danda.
Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Mohamed Gombati amewaongoza waombolezaji katika shughuli ya kuiaga miili miwili Nyumbani kwa marehemu Danda huku Askof wa manisa ya TAG Saimon Masunga akiwataka waumini wa kanisa hilo na madhehebu mengine kujiandaa.