Kero ya barabara yawazidia wana Kilimbu, Msalala
8 October 2023, 3:04 am
Licha ya ahadi kadhaa kuendelea kufanyiwa kazi kwa wananchi wa Msalala lakini bado kero ya barabara ni kubwa katika kijiji cha Kilimbu.
Na Zubeda Handrish- Msalala
Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi akiwa katika kijiji cha Kilimbu kata ya Mwalugulu, Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ameendelea kukutana na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi wake.
Katika mkutano huo wa hadhala wananchi wametoa kero zao ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara.
Nae Diwani wa kata ya Mwalugulu ameelezea jitihada zinazofanyika katika kuendelea kuleta maendeleo na kuwakwamua wananchi kutoka katika changamoto hizo.
Nae Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi amejibia changamoto walizotoa wananchi na suluhisho lake.