Mgodi wa Buckreef walipa fidia kwa wananchi
14 September 2023, 12:50 pm
Mgodi wa Buckreef umechukua eneo la wananchi wa Lwamgasa lenye kilomita za mraba 12 kwa ajili ya kupanua shughuli za uzalishaji wa mgodi huo.
Mgodi wa Uchimbaji madini ya dhahabu wa buckreef uliopo kata ya Lwamgasa Jimbo la busanda wilaya ya Geita umesema tayari umeshalipa fidia kwa wananchi 983 waliopisha upanuaji wa mgodi sawa na asilimia 98 .2 ya watu wanaopaswa kulipwa fidia ya kwa ajili ya kupisha eneo hilo.
Hayo yameelezwa na Meneja Usimamizi wa Mgodi, Gaston Mujwahuzi wakati akifafanua mchakato huo wa ulipaji wa fidia kwa wanachi wa eneo hilo mbele ya mkuu wa mkoa wa Geita Martini Shigella alipofika mgodini hapo kujionea uwekezaji.
Mgodi ulipanga kulipa kiasi cha sh billioni 6.3 kwa wananchi wote ambapo bilioni 6.2 ndo imetumika kulipa na kubakia asilimia mbili kwa watu ambao hawajafika kuchukua fedha zao, huku Mjiolojia wa Mgodi huo Isack Disasaba akizungumza.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Martini Shigela ameupongeza mgodi wa Buckreef kwa kuonyesha mfano sambamba na kuwa kinara wa ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo.
Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani anaendelea kuwekà mazingira rafiki ya uwekezaji lakini hataki kuona watu wanaonewa kwa kulipwa fidia au kwa njia yoyote huku akiwaomba migodi mingine kufuata njia walizofanya bucreef kwa wananchi wa Lwamgasa.