Vyombo vya maamuzi kikwazo mapambano dhidi ya ukatili Geita
12 September 2023, 9:02 pm
Na Mrisho Sadick – Geita
Naibu waziri wa maendeleo ya Jamii , jinsia, Wanawake na makundi maalumu Mwanaidi Ali Khamis amevitaka vyombo vya kutoa maamuzi kuharakisha uchunguzi nakutoa uamuzi wa kesi mbalimbali za vitendo vya ukatili ili kuepuka kupoteza ushahidi na watuhumiwa kuachiwa huru.
Mhe Mwanaidi Ali Khamis ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa serikali ya Mkoa wa Geita katika ziara yake Mkoani humo ya kufuatilia tathimini ya Utekelezaji wa sera , sheria na miongozo mbalimbali inayotekelezwa na wizara hiyo.
Baadhi ya Wananchi Mkoani Geita Ester Robert na John Daud wamesema kutotolewa haraka kwa maamuzi ya kesi za vitendo vya ukatili inawakatisha tamaa.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mwanaid Ali Khamis ametembelea vikundi vya wanawake vya uzalishaji na Uchumi nakusifu jitihada hizo huku akisema serikali itawaunga Mkono katika mapambano hayo.