Vibubu vyaboreshwa kuendana na soko
21 August 2023, 9:06 am
Inadaiwa kibubu hakiwezi kutoa usalama wa moja kwa moja kama benki, huku kikidaiwa kupoteza fedha zilizohifadhiwa ndani yake , hili limewainua wauza vibubu na kutolea ufafanuzi.
Na Zubeda Handrish- Geita
Mfanyabiashara wa Vibubu katika soko la Nyankumbu la jioni amezungumzia namna vibubu vinavyonunuliwa kwa wingi katika eneo lake na zaidi wanawake wakivunja rekodi.
Kutokana na kukua kwa soko la Vibubu kwa kununuliwa na watu wa kaliba tofauti, baadhi ya wabunifu wameviongezea thamani zaidi kwa kuvitengeneza kwa muonekano wa kuvutia.
Nao baadhi ya wananchi mjini Geita, wamesemaje wanatumia vibubu ili kuwekeza pesa kidogo kidogo kwaajili ya kutimiza malengo yao.
Tukamilisha hapa na meneja wa moja ya benki mjini Geita akielezea umuhimu wa kutunza pesa katika taasisi za kifedha hususani benki.
Ili kuepuka madhara haya, ni bora kuweka fedha zako katika taasisi za kifedha zilizosajiliwa kisheria, kama vile benki. Benki zinatoa usalama zaidi na fursa za uwekezaji na faida zingine.
Kama unataka kuwekeza au kufanya uwekezaji wa muda mrefu, unaweza pia kuzingatia chaguzi za uwekezaji zilizoainishwa vizuri na wataalamu wa kifedha.