Dira ya Taifa ya 2025 yawa na mafanikio makubwa Geita
21 July 2023, 11:30 am
Wakati Dira ya Taifa ya mwaka 2025 ikiwa inaelekea ukingoni, wananchi mkoani Geita wameeleza mafanikio makubwa huku wakiipongeza serikali kwa kuwashirikisha.
Na Mrisho Sadick
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 inayotegemewa kumalizika 2025 imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kusogeza mbele maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, huduma za afya, miundombinu, maji pamoja na maendeleo kiuchumi.
Hayo yameelezwa na wakazi wa halmashauri ya mji wa Geita katika hafla ya maandalizi ya ukusanyaji wa maoni ya dira ya taifa 2050 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa EPZA.
Omary Othman kiongozi kutoka Wizara ya Fedha anasema serikali inakuja na zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi kwa ajili ya kuandaa Dira ya Taifa ya mwaka 2050.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanza mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya dira ya mwaka 2050 kwa kuwashirikisha wananchi.
Malengo makuu ya Dira ya Taifa 2025 ilikuwa ni kufikia uchumi wa kati na kuwa na taifa lenye hali bora ya maisha kwa watu, amani, umoja na utulivu, uongozi bora , jamii iliyoelimika na uchumi wenye ushindani.