Wahitimu vyuo vya Biblia watakiwa kuisaidia jamii
10 July 2023, 3:35 pm
Wahitimu wa vyuo mbalimbali vya Biblia wa Muungano wa makanisa ya Kipentekoste Tanzania wametakiwa kutumia ujuzi na elimu ambayo wanaipata kwenye vyuo hivyo kuisaidia jamii.
Na Kale Chongela:
Askofu Mkuu wa makanisa ya kipentekoste Tanzania Eliaza Issack amewataka wahitimu wa vyuo vya Biblia kutumia elimu yao katika kukemea ushoga na kufundisha watu kuifuata njia ya kweli katika imani.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la ( MMPT ) katika kanisa la Pentkoste lililopo mamlaka ya mji mdogo wa Katoro alipokuwa akiwahusia wanafunzi ambao wamehitimu chuo cha biblia uyovu tawi la Katoro.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa chuo cha biblia wameahidi kuwa tayari kuitumikia jamii kwa kuhubiri habari njema kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vitakatifu.
Aidha Mkurugenzi wa Chuo cha Biblia Mchungaji Elifazi John amesema wahitimu kwa ngazi ya Astashahada ni 13 kati ya hao mwanamke ni mmoja na ngazi ya Cheti 17.