Kupokea rushwa ni kosa, toa taarifa
5 July 2023, 11:25 am
Suala la kutoa na kupokea rushwa kwa viongozi na wafanyakazi wa sekta binafsi na za serikali mkoani Geita bado limeonekana kuwa ni changamoto na kupelekea Kaimu Kamanda Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita kuzungumzia hilo.
Na Kale Chongela -Geita
Naibu Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita Aza Mtaita wakati akizungumza na Storm FM Ofisini kwake Julai Mosi, ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya rushwa.
Amezungumza hayo baada ya Kesi 13 kutoka sekta mbalimbali kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita na Mahakama ya Wilaya ya Geita, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.