Kichanga cha siku 2 chakutwa kimefariki katika dampo la uchafu.
6 January 2023, 10:03 am
Na Kale Chongela:
Katika hali ya kusikitisha kichanga kilichokadiliwa kuwa na siku mbili kimekutwa kimefariki dunia katika dampo la uchafu lililopo katika uwanja wa CCM kalangalala mjini Geita.
Kaimu kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokaji mkoani Geita Inspekta Edward Lukuba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema uchunguzi wa awali imebainika kuwa mtoto huyo amekutwa akiwa amefariki dunia na kwamba jitihada za kumtafuta aliyetenda kosa hilo zinaendelea.
Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda wamesema eneo hilo ni kwa ajili ya kutunza taka ngumu lakini katika hali ya kusikitishwa alionekana mwanaume akiwa na mfuko uliokuwa ukionekana kuwa ni taka ngumu na baada ya kwenda kwenye dampo hilo imeonekana kuwa ni kichanga kimetupwa.