Storm FM

Serikali yaahidi kuendeleza ushirikiano na viongozi wa dini

12 December 2022, 2:26 pm

                  

                                                                                                              Waziri wa Madini Mhe Dotto Biteko

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Dini hapa nchini kwakuwa wamekuwa msaada katika  kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na kupambana na vitendo vya Ukatili wa kijinsia katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Madini Mhe Dotto Biteko katika hafla ya Kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Tatu wa Kanisa la  African inland Church (AICT) Dayosisi ya Geita, Bw Reuben Yusuph Ng’wala katika viwanja vya Yeriko mjini Geita.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela ameahidi kushirikiana na Askofu huyo Mpya ambapo amesema anatambua kuwa mchango wa viongozi wa dini katika Mkoa wa Geita ni mkubwa nakwamba hatakuwa kikwazo kwao.

Baada ya zoezi la kuwekwa wakfu nakusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Geita, Reuben Ng’wala amesema wataendelea kuombea mipango yote ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali, huku Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Mussa Magwesela akiwataka watumishi wake  kuendelea kufundisha neno la mungu kwa kufuata misingi ya Kanisa hilo.

.

 

                                                              Askofu Reuben Ng’wala mbele nyuma ni Askofu Mkuu wa AICT Tanzania Mussa Magwesela