Mradi wa magari ya umeme mbioni kuanza.
11 March 2022, 5:34 pm
Na Joel Maduka:
Imeelezwa kuwa, Kampuni ya Peak Resources Ngualla (PRNG) itakayo jihusisha na uchimbaji wa madini ya teknolojia ya Rare Earth Elements ipo katika hatua za mwisho za makubaliano na serikali ili ianze uchimbaji wa madini hayo.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa mara baada ya kutembelea eneo linalotarajiwa kufunguliwa mradi huo lililopo katika kijiji cha #Ngwala wilaya ya Songwe.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wanakijiji wa #Ngwala Dkt. Kiruswa amewatoa wasiwasi wananchi wa kijiji hicho ambao wana shauku kubwa ya kuona mradi huo unaanza uzalishaji ili wapate fursa mbalimbali za kiuchumi ambapo amesema kuwa, Serikali ipo katika hatua za mwisho za makubaliano na kampuni hiyo.
Aidha, Dkt. Kiruswa amesema mradi huo ukianza uzalishaji utakinufaisha kijiji cha #Ngwala na mkoa wa #Songwe pamoja na taifa kwa ujumla kutokana na umuhimu wa madini hayo ambayo hutumika kutengenezea simu, vifaa vya umeme ikiwemo magari yanayo tumia umeme.15m