Wafugaji wakaidi kuchukuliwa hatua kali Geita
14 April 2021, 4:02 pm
Na Kale Chongela
Serikali ya mtaa wa Tambukareli kata ya kalangalala Halmashauri ya mji wa Geita imeanza utekelezaji wa kuwachukulia hatua kali wafugaji ambao hawazingatia taratibu na kanuni za ufugaji maeneo ya mjini.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw Mabula Ndoshi akizungumza na Storm FM Ofisini kwake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima wanaodai kuharibiwa mazao yao na mifugo , amesema kumekuwepo na baadhi ya wafugaji ambao hawazingati taratibu na kanuni za ufugaji hali ambayo inasababisha malalamiko mengi baina ya wakulima na wafugaji nakwamba ofisi yake itaendelea kuchukua hatu kali ili kuodoa changamoto hiyo.
Miongoni mwa wakulima walioharibiwa mazao yao na mifugo nakufika katika ofisi ya serikali ya mtaa huo Bw Mwembeki Dickson amesema mazao yake mahindi , marando ,mihogo na migomba yameharibiwa vibaya na mifugo aina ya Ngo’ombe na Mbuzi nakuuomba uongozi wa mtaa huo kuingilia kati kutatua mgogoro huo.
Aidha baadhi ya wafugaji katika mtaa huo wamekiri kuwepo kwa changamotyo hiyo nakuahidi kuendelea kuzingatia taratibu na kanuni za ufugaji zilizopo ili kuepukana na migogoro hiyo.