Mnyama aina ya kima azua taharuki Geita
8 April 2021, 12:23 pm
Na Mrisho Sadick
Mnyama aina ya kima au mbega amezua taharuki katika Mtaa wa uwanja mjini Geita baada ya kuingia katika makazi ya watu huku akiwa hajulikani ametoka wapi.
Kima akiwa amejificha chooni
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wakazi wa Mtaa huo walioingiliwa na mnyama huyo wamesema aliingia katika nyumba yao baada ya kufukuzwa na watoto pamoja na mbwa kitendo kilichomfanya kuwa mkali na tishio kwa usalama wa maisha ya watu.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Uwanja Bw Enos Chelehan alifika eneo la tukio na jitihada za kumuondoa ziligonga mwamba hadi pale alipo watafuta maafisa uhifadhi wa wanyapori kwenda kumuondoa mnyama huyo.
Zoezi la kumuondoa Kima huyo lilichukua takriba masaa mawili kutoka kwa maafisa uhifadhi pamoja na wananchi wa mtaa huo. Na baada ya kumtoa ndani ya choo alikokuwa amejificha maafisa uhifadhi wanyapori walimpeleka katika hiafdhi ya pori la Samina.