Mazingira FM

Recent posts

24 August 2026, 10:50 am

Kibe: Serikali itoe mapema mwongozo wa uuzwaji wa mbegu

Kumekuwepo changamoto kwa wakulima kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi na mwongozo kuhusu mfumo wa ununuzi wa mbegu katika msimu huu. Na Adelinus Banenwa Wito umetolewa kwa Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa uuzaji wa mbegu katika msimu mpya wa kilimo…

24 August 2026, 6:33 am

Wanafunzi Makongoro waomba haki itendeke kifo cha mwenzao

Wanafunzi hao wamekanusha taarifa kwamba mwanafunzi huyo alipigwa fimbo mbili pekee, wakidai kuwa alichapwa na walimu kadhaa, huku wakitaja idadi ya takribani walimu 30. Na Adelinus Banenwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongoro, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani…

23 August 2026, 8:44 pm

Wananchi watakiwa kutoa ushahidi wa ukatili wa kijinsia

Wananchi wanapaswa kutambua kuwa kutoa ushahidi wa tukio la ukatili wa kijinsia ni sehemu ya kumsaidia mwathirika kupata haki Na. Edward Lucas Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria kwa kutoa ushahidi wa matukio ya ukatili wa kijinsia wanapohitajika,…

23 August 2026, 3:22 pm

Ukeketaji unavyochangia ndoa za utotoni

Asilimia 38.3 ya wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 mkoani Mara walikuwa wameolewa kabla ya kufikisha miaka 18. Na Edward Lucas Baadhi ya mila zinazohusisha ukeketaji mkoani Mara zimeelezwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia wasichana kuingia kwenye ndoa…

22 August 2026, 6:51 pm

Wakili Alloyce: Andikeni wosia kuepusha migogoro

Sababu zinazoweza kumfanya mwenye mali asimjumuisha mtoto ni pamoja na mtoto kutomuhudumia mzazi wakati akihitaji msaada au kuwa na kusudio la kumuua mzazi kwa lengo la kupata mali. Na Adelinus Banenwa Wito umetolewa kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuandika wosia…

21 August 2026, 10:18 am

Bodi ya pamba yawapiga msasa wanahabari Kanda ya Ziwa

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya pamba iwapo vitatumika vizuri na kutoa taarifa sahihi kwa wakulima na wadau wengine Na Angel Mbalamwezi Bodi ya Pamba Tanzania kwa kushirikiana na STV Online imetoa mafunzo kwa waandishi…

20 August 2026, 9:27 pm

Walimu sita mbaroni kifo cha mwanafunzi Bunda

Hadi sasa walimu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi, huku uchunguzi wa kitabibu ukisubiriwa ili kubaini chanzo halisi cha kifo. Na Adelinus Banenwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, amethibitisha kifo cha mwanafunzi…

20 August 2026, 9:59 am

Mwanafunzi afariki baada ya kudaiwa kuchapwa fimbo na walimu 8

Adhabu ya kuchapwa fimbo ilitolewa kwa wanafunzi na walimu waliokuwa katika foleni Taharuki imetanda katika Shule ya Sekondari Makongoro, Wilaya ya Bunda, baada ya mwanafunzi wa kidato cha sita, Peter Maira (19), anayedaiwa kufariki baada ya kupewa adhabu ya kuchapwa…

19 August 2026, 6:22 pm

Changamoto ugawaji vyandarua Saranga watua kwenye kikao cha mtaa

Miongoni mwa kero zilizowasilishwa ni zoezi la ugawaji wa vyandarua vilivyotolewa na Serikali. Na Juma Hangi Wakazi wa Mtaa wa Saranga wamewasilisha kero mbalimbali zinazowakabili katika kikao kilichofanyika Agosti 18, 2026, kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo, Philipo Safari, kwa…

19 August 2026, 11:46 am

‘Hii ndiyo miezi hatari kwa ukeketaji Mara’

Kwa baadhi ya jamii mkoani Mara, miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba hutajwa kuwa kipindi cha hatari, ambapo vitendo vya ukeketaji huongezeka. Na Edward Lucas Wadau wa kupambana na ukatili wa kijinsia mkoani Mara wametaka mikakati ya kuzuia ukeketaji kuanza…

Ifahamu Mazingira FM

Mazingira FM ni kituo cha radio chenye maudhui ya kijamii,kilichoanzishwa Mwaka 2011.
Mazingira fm inatangaza kutoka maeneo matatu (3) ndani ya mkoa wa mara ili kuwa na usikivu wa uhakika, ambapo Mnara mkuu upo wilaya ya Bunda, na mingine ipo wilaya ya Tarime na Musoma
Usikivu.


Mazingira fm inasikika katika wilaya zote za mkoa wa Mara, Bunda, Musoma,Tarime, Serengeti, Rorya na Butiama na kwa mkoa Simiyu inasikika katika wilaya za Busega, Bariadi, Maswa na Itirima kwa Mkoa wa mwanza inaskika katika wilaya za magu,ukerewe, kwimba na misungwi.

Muundo wa vipindi 70% mazungumzo na 30% ya muziki katika matangazo ya kila siku.

Mawasiliano.
P.o box 51
Saranga, kabarimu, Bunda
Postcode-31530
Tel:0621046491
mazingirafm@gmail.com
https://radiotadio.co.tz/mazingirafm/
www.mazingirafm.com