Fumanizi laua asiyetarajiwa kijiji cha Bugalama
4 November 2024, 12:54 pm
Wivu wa mapenzi umeendelea kusababisha vifo kutokana na maamuzi ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi mkoani Geita.
Na: Evance Mlyakado – Geita
Kijana Faida Deusi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25-35 mkazi wa kijiji cha Bugalama kata ya Bugalama wilayani Geita amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mwanaume ambaye hakufahamika jina lake mwenyeji na mkazi wa kijiji cha Kamhanga kutokana kile kilichotajwa kuwa Mwanaume huyo alifika kijiji cha Bugarama kwa lengo la Kumfumania mwanaume mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Mika ambaye pia ni mwenyeji na mkazi wa kijiji cha Kamhanga ambapo Mika anadaiwa kusababisha mwanaume huyo kutengana na mke wake.
Wakizungumza na Storm fm, ndugu wa mwanamke huyo wamesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 30, 2024 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Bugalama.
Dotto Luhuyege ni kaka wa marehemu Faida Deus akizungumza kwa njia ya simu amesema kuwa alipigiwa majira ya saa saba usiku na kupatiwa taarifa za tukio hilo kisha kuchukua uamzi wa kuelekea eneo la tukio.
Balozi wa eneo Elisha William amesema mwanamke huyo alitoka kwa mume wake katika kijiji jirani cha Kamhanga kisha kurejea nyumbani kwa ndugu yake, huku akitupa lawama kwa viongozi wa ngazi za juu kutokana na kushindwa kushughulikia migogoro mbalimbali ya kifamilia wakati inapojitokeza hali inayopelekea kukithiri kwa vitendo vya ndoa kuvunjika.