

3 April 2025, 6:49 pm
“Mazao, miundombinu ya umeme, vimeharibiwa na huu mtambo licha ya kujeruhi watu” – Mwananchi
Na: Edga Rwenduru:
Watu watano kutoka katika kaya tatu zilizopo kitongoji cha Isingilo, kata ya Lwamgasa mkoani Geita wamejeruhiwa vibaya baada ya mtambo unaotumika katika uchimbaji wa madini katika mgodi wa dhahabu wa Buckreef kugonga na kuharibu nyumba tatu za wakazi wa kitongoji hicho.
Mashuhuda ambao pia ni waathirika wa tukio hilo Charles Mhoja na Mariam Kasandiko wamesema licha ya kujeruhi watu pia limesababisha uharibifu wa nyumba, miundombinu ya umeme ,mazao pamoja na chakula.
Mwenyekiti wa kijiji cha Lwamgasa Mwita Chacha Amos amesema kwa taarifa alizozipata ni kwamba trekta hilo lilitoka maeneo ya mgodi likiwa halina dereva anayeliongoza
Akitolea ufafanimuzi wa nini sababu ya kutokea kwa tukio hilo Afisa habari wa Mgodi wa Bakreef Amelda Msuya amesema ajali hiyo imesababishwa na Dereva yaani Operator aliyekuwa akijaribu kuiba mafuta.