Storm FM

Jeshi la polisi lawatahadharisha wananchi kulewa kupita kiasi

23 December 2024, 4:20 pm

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Geita Mrakibu wa jeshi la polisi Aloyce Jacob. Picha na Edga Rwenduru

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani Geita limetoa rai kwa wananchi kutotumia vilevi kupitiliza katika msimu huu wa mwisho wa mwaka.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Geita kimewataka wananchi wanaolewa kupita kiasi kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kuacha taibia hiyo kwani wengi husababisha ajali wakati wakivuka barabara.

Akizungumza na Storm fM Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Geita Mrakibu wa jeshi la polisi Aloyce Jacob Disemba 21, 2024 ambapo amesema mara kadhaa watu wanaokunywa pombe kupitiliza kipindi hiki cha sikukuu wamekuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani.

Sauti ya RTO Geita

Mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Geita wakati wameendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika kituo kikuu cha mabasi ya abiria mjini Geita ambapo wamesema wamegundua idadi kubwa ya magari yasiyokuwa na mikanda na yanayozidisha kiwango cha nauli kwa abiria.

Sauti ya mabalozi wa usalama
Utoaji wa elimu kwa madereva na abiria ukiendelea katika kituo cha mabasi ya abiria mkoani Geita. Picha na Edga Rwenduru

Afisa habari wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Sajenti Bahati Lugodisha amesema wamebaini magari mengi yanayofanya safari za ndani na nje ya mkoa wa Geita hayana vifaa vya kuzimia moto kama wanavyoelekezwa.

Sauti ya Sajenti Bahati Lugodisha
Utoaji wa elimu kwa madereva na abiria ukiendelea katika kituo cha mabasi ya abiria mkoani Geita. Picha na Edga Rwenduru