Storm FM

Mtoto (3) afariki dunia kwa kutumbukia kisimani Geita

26 September 2024, 10:17 pm

Zoezi la kufunika shimo ambalo limesababisha kifo cha mtoto baada ya kutumbukia. Picha na Edga Rwenduru

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu amefariki dunia kwa kutumbukia katika kisima baada ya kudaiwa kutoweka nyumbani na kisha kukutwa ndani ya kisimani.

Na: Ediga Rwenduru – Geita

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu aliyetambulika kwa jina la Junior Mussa Pius amefariki dunia baada ya kutumbukia katika kisima cha maji katika kitongoji cha Nyampa kijiji cha Kasamwa wilayani na mkoani Geita.

Wazazi wa mtoto huyo wamesema  tukio hilo lililotokea asubuhi ya Septemba 24, 2024  na wakati tukio hilo linatokea mtoto wao alikuwa ametoweka nyumbani ndipo wakataarifiwa kuwa ametumbukia kisimani na kufariki dunia.

Sauti ya wazazi
Mama mzazi wa mtoto, aitwaye Neema Charles akizungumzia tukio la mtoto wake kufariki dunia. Picha na Edga Rwenduru

Mwenyekiti wa mtaa hicho cha Nyampa Helena Maneno amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akisema Jeshi la polisi limefanikiwa kufika katika eneo la tukio.

Sauti ya Mwenyekiti wa kitongoji

Pichani ni Mwenyekiti wa mtaa wa Nyampa Helena Maneno. Picha na Ediga Rwenduru

Juhudi za kumtafta kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Geita zinaendelea ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu tukio hilo.