Storm FM

Wazee Geita watoa neno mfumo wa elimu nchini

26 September 2024, 3:47 am

Umoja wa wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Mpomvu mwaka 1973-75 wamekutana kuadhimisha miaka 50 tangu kuhitimu elimu hiyo.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Baadhi ya wazee waliohitimu katika shule ya msingi Mpomvu wamependekeza kufanyika marekebisho katika mfumo wa elimu unaotumika kwa sasa kutokana na madai kuwa mfumo huo haumuandai mwanafunzi kuelewa bali unamjengea uwezo wa kukariri anachofundishwa.

Wameeleza hayo Septemba 25, 2024 katika hafla ya kupongezana kufikisha miaka 50 tangu kuhitimu elimu ya msingi na kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini, hafla iliyofanyika kijiji cha Nyakamwaga kata ya Nyakamwaga wilayani na mkoani Geita.

Sauti ya wazee

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mwl Lenard Singu (92) ambaye ndiye aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa wakati huo amesema serikali inatakiwa kufanya mabadiliko katika sera na mitaala ya elimu ili kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea.

Sauti ya mgeni rasmi