Polisi Geita: Mikopo ya pikipiki iende sambamba na mafunzo ya udereva
7 November 2023, 6:30 pm
Ajali za barabarani zaliibua Jeshi la Polisi juu ya mikopo holela ya pikipiki kwa vijana isiyozingatia usalama wao.
Na Mrisho Sadick – Geita
Jeshi la Polisi mkoani Geita limezitaka kampuni na watu binafsi wanaotoa mikopo ya pikipiki kwa vijana kuingia makubaliano na vyuo vya mafunzo ya udereva ili vijana wanaoomba mikopo hiyo waweze kupatiwa mafunzo kabla ya kupewa vyombo hivyo ili kupunguza ajali za barabarani.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani mkoa wa Geita Mrakibu wa Polisi Joachim Aloyce wakati akizungumza na viongozi wa umoja wa waendesha Pikipiki Mkoa wa Geita ili kubaini changamoto zinazowakabili huku mwenyekiti wa umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Geita Carlos Ndagiwe akiomba mchakato huo uanze haraka ili kuwasaidia vijana.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha mapinduzi CCM Wilaya ya Geita Michael Msuya amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya sita nikuweka Mazingira rafiki kwa waendesha Pikipiki hapa nchini.