Taulo za kike za kushona mkombozi kwa familia masikini
17 August 2023, 12:35 pm
Kundi la watoto wa kike hususani maeneo ya vijijini mkoani Geita linakatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya hedhi.
Na Mrisho Sadick:
Ujuzi wa kushona taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani Geita umekuwa mkombozi kwa familia zisizo na uwezo wa kumudu gharama za kununua taulo hizo kila mwezi.
Liliani Michael mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mwatulole mjini Geita ambaye anatoka familia ambayo haina uwezo wa kumudu gharama za kununua taulo za kike kila mwezi , amepata ujuzi wa kushona taulo hizo Kutoka shirika la Marafiki wa Elimu lenye makao yake mkoani Geita.
Msimamizi wa miradi wa shirika la marafiki wa elimu Amina Mvungi amesema wanafunzi wa kike wanaotoka familia duni wengi wamekatisha masomo huku wengine wakiwa watoro wanapokuwa katika kipindi cha Hedhi kwakuwa wanakosa uhuru.
Mkurugenzi wa Shirika la marafiki wa Elimu Mkoani Geita Ayobu Bwanamadi anasema wameendelea kutoa elimu katika makundi tofautitofauti ikiwemo ya wanafunzi na mtaani kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike kukabiliana na changamoto hiyo.