Storm FM

Wakazi wa Nshinde walia na ubovu wa barabara

23 December 2024, 4:06 pm

Muonekano wa barabara katika mtaa wa Nshinde mjini Geita baada ya kuharibiwa na mvua. Picha na Kale Chongela

Baadhi ya miundombinu ya barabara katika mitaa na maeneo mbalimbali mkoani Geita imeendelea kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Na: Kale Chongela – Geita

Wakazi wa mtaa wa Nshinde kata ya Nyankumbu mjini Geita wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayosababisha changamoto katika utumiaji wa barabara hiyo.

Wamebainisha hayo leo Disemba 23, 2024 wakizungumza na Storm FM kuwa ubovu wa barabara hiyo umesababaisha kutumia gharama kubwa ya nauli kwani  hulazimika kuzunguka pindi wanapohitaji kwenda Nshinde senta kwaajili ya kupata mahitaji mbalimbali.

Sauti ya wananchi
Muonekano wa barabara katika mtaa wa Nshinde mjini Geita. Picha na Kale Chongela

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nshinde Bw. Edward Malimi ameeleza kuwa licha ya kutoa taarifa juu ya ubovu huo wa barabara kwa TARURA  bado hakuna hatua wala mafanikio yeyote ya kuirekebisha

Sauti ya mwenyekiti

Kaimu meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) wilaya ya Geita Mhandisi Cathbet Robert amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya ubovu wa barabara na kueleza hatua zilizopo katika kutatua changamoto hiyo.

Sauti ya kaimu meneja TARURA