GGML yakabidhi nyumba 6 na pikipiki 50 kwa jeshi la polisi Geita
7 October 2024, 10:10 am
Mgodi wa Geita Gold Minning Limited umekabidhi nyumba 6 na pikipiki 50 kwa Jeshi la polisi mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya urejeshaji wa Jamii (CSR).
Na: Evance Mlyakado – Geita
Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko Oktoba 05, 2024 amezindua nyumba sita zenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 zilizojengwa na mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa GGML kwaajili ya makazi ya maafisa wa Jeshi la polisi.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita SACP Safia Jongo ameeleza tathmini na taarifa ya utekelezaji wa mradi huo
Makamu wa Raisi wa Anglo Gold Ashanti Afrika, Simon Shayo amesema nyumba hizo zilizopo katika mtaa wa Magogo kata ya Bombambili wilayani Geita ni sehemu ya Urejeshaji wa GGML Kwa Jamii (CSR)
Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Doto Mashaka Biteko ambaye alikuwa mgeni rasmi ameipongeza wizara ya madini kwa usimamizi mzuri wa sheria mbalimbali za madini ambazo zimesaidia Kwa kiasi kikubwa kuchochea ukuaji wa maendeleo katika maeneo mbalimbali.