Storm FM
DC Geita Awasisitiza Wakulima Kuchangamkia Fursa Za Mikopo.
31 May 2021, 8:16 pm
Na Joel Maduka:
Mkuu wa wilaya ya Geita Fadhili Juma amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya Mkopo wa vifaa vya Kilimo inayotolewa na Benki ya NMB ambayo itawasaidia kujikwamua kwenye shughuli zao za kilimo ambazo wamekuwa wakizifanya.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhili Juma ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza kwenye Washa ya siku moja iliyoandaliwa na beki ya NMB tawi la Geita iliyokuwa imelenga kuelekeza fursa ambazo wakulima wanaweza kufaidika nazo kutoka kwenye Benki hiyo.
Amesema ni kipindi mahususi wakulima kutumia kilimo biashara ambacho kitawasaidia kuinuka kiuchumi na kuachana na kilimo cha mazoea.