Storm FM

Watu wawili wanusurika kifo kwa ajali mbaya ya ya pikipiki

19 September 2024, 12:16 am

Pichani ni umati wa watu wakiwa eneo la tukio.picha na Kale chongela.

Katika hali ya kushangaza dereva pikipiki na dereva baiskeli wamegongana na kusababisha watu wawili kunusurika na kifo wakiwa katika shughuli zao za kila siku za kusafirisha abiria.

Na Kale chongela.

Watu wawili wamenusurika kifo baada ya ajali ya dereva pikipiki na mwendesha baiskeli iliyotokea mtaa wa mwatulelo kata ya Buhalahala Mjini Geita

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa mwendesha baiskel alikuwa akitoka mjini Geita  kuelekea mtaa wa mwatulole kwa ajili ya kuchukua soda wakati akijaribu kukata kona kwenda eneo la kuchukua soda  ndipo dereva pikipiki akamgonga  upande wa mkono wa kulia

Ni sauti ya baadhi ya mashuhuda walioshuhudia tukio hilo

Pichani ni baadhi ya wananchi wakishuhudia baada ya majeruhi kuchukuliwa.picha na Kale chongela.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Mrakbu Hamisi Shabani Dawa ametibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa tukio hilo limetokea septemba 18 na kwamba majeruhi wametambulika kwa jina la  Hamanye  Anasiasi ambaye ni dereva  pikipiki na  chibanya Juma  mwendesha baiskeli.