Wananchi Wigembya na Ikulwa waanza kupata maji safi
15 July 2024, 10:44 am
Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba ameendelea kutembelea wananchi katika maeneo mbalimbali ya wilaya yake ambapo ameweka jiwe la msingi katika mradi maji uliopo Wigembya.
Na: Kale Chongela – Geita
Zaidi ya wananchi elfu kumi na tatu mia nne 13,000 wameanza kupata huduma ya maji safi na salama katika kijiji cha Wigembya kata ya Ihanamilo mjini Geita.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Julai 13, 2024 mhandisi Yohana Masheria kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita (GEUWASA) ambao wamehusika na ujenzi wa mradi huo akiwa katika kijiji cha Wigembya kata ya Ihanamilo halmashauri ya mji wa Geita amesema mradi huo umekuwa chachu katika kuongeza jitihada za maendeleo kwa wananchi wa Ikulwa na Wigembya
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Wigembya na Ikulwa wamesema mradi huo umekuwa na tija kwao tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Mkuu wa wilaya ya Geita Hashimu Komba ambaye ameweka jiwe msingi katika mradi wa maji Wigembya ambao umegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 32 ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kulinda miundombinu ya maji.