Tumekuja kuinua soka la wanawake
4 May 2021, 6:55 pm
Na Mrisho Sadick:
Mwenyekiti wa Chama cha Soka la wanawake Mkoani Geita Mwalimu Veronica William ameahidi kuinua soka la wanawake Geita kwa kuanza na shule za Msingi.
Amesema hayo siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho nakuahidi kuuinua mkoa wa Geita katika soka la wanawake ambapo ameiomba jamii kumpa ushirikiano ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wake mhazini wa chama hicho Bi Kwimba Hilu amesema watahakikisha wanapata ofisi haraka ili kuanza kushughulika na masuala ya soka la wanawake mkoani Geita.
Viongozi wengine waliochaguliwa kukiongoza chama cha mpira wa miguu wanawake mkoani Geita ni Ludigardes Abel Makamu mwenyekiti, Elizabeth Mwangonera Katibu Mkuu, Mgeni Ayubu Katibu Msaidizi, Jonisia Makalo Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa.