Wakazi mtaa wa Uwanja waomba shule ya upili (sekondari)
2 May 2024, 4:13 pm
Licha ya jitihada za serikali kuwekeza katika elimu kwa kujenga shule mpya na za kisasa kwa baadhi ya maeneo nchini, bado ni kitendawili kwa wakazi wa mtaa wa Uwanja kutokana na kukosa shule ya upili (sekondari).
Na: Edga Rwenduru – Geita
Wakazi wa mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita wameiomba serikali kuwajengea shule ya sekondari katika mtaa huo kwani watoto wao wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule ya sekondari Rukaranga.
Wamebainisha hayo katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya katibu mwenezi na mafunzo wa tawi hilo Sebastian Kanga wakieleza kuwa wanalazimika kuingia gharama za kuwalipianauli ya daladala kwenda na kurudi.
Aidha katika hatua nyingine wananchi hao wameiomba serikali kuwatengenezea barabara za mitaa ambazo zimeharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mwenyekiti wa mtaa huo Enos Chelehani pamoja na Katibu mwenezi CCM tawi la uwanja Sebastiani Kanga wamesema tayari mtaa umeanza kuchukua hatua za kufanyia kazi changamoto hizo.